Huduma za Tafsiri Afrika Kusini

Karibu katika Kampuni yetu inayotoa huduma za tafsiri za kitaalamu Afrika Kusini. Tumedhamiria kutoa huduma bora za tafsiri zenye maudhui ya kibiashara, kisheria na kiafya katika lugha rasmi 11 za Afrika Kusini. Pia, tunatoa huduma za tafsiri kwa wabia wakuu wa kibiashara wa Afrika Kusini katika lugha za Kireno, Kihispania, Kijerumani, Kiswahili na Kichina Kimandarini. Tafsiri zetu zote zinakidhi viwango vya tafsiri vya kimataifa.

Angalia kiwango cha tafsiri zetu. Kurasa za wavuti za Kiingereza na zile zilizojanibishwa zinafanana. Tafsiri zetu zinaeleweka kwa urahisi na hazina makosa ya kitahajia katika huduma zetu zote za lugha za Afrika Kusini.

Chagua lugha mojawapo hapa chini ili uingie katika wavuti yetu kwa kutumia lugha yako:

This browser does not support the video element.

Ubora: Pata kilicho bora mapema

Kazi zetu hufanywa na wafasiri waliobobea tu. Tunapofasiri waraka wa kisheria, tunamtumia mfasiri wa matini za kisheria anayetumia lugha ya kwanza. Kiwango cha chini cha masharti ya kitaaluma ni kukidhi vigezo vya vyuo vikuu vya Afrika Kusini. Aidha, kiwango cha chini cha wafasiri wetu ni uzoefu wao wa kazi uliotukuka usiopungua miaka 10. Daima tunapenda kutoa sifa za kitaaluma, na kutia saini Mkataba wa Viwango vya Huduma ili kudhihirisha ubora wa tafsiri zetu.

Kupitia tahajia katika MS Word

Nyaraka zako zilizotafsiriwa huhaririwa kwa uangalifu mkubwa kama matini ya Kiingereza. Aidha, tunatumia kompyuta kuhakikisha kuwa nyaraka zako hazina makosa ya kitahajia, zinatumia lugha ya kisasa na zinashughulikiwa kwa usawa. Tunafurahia kulidhihirisha hili.

Makataa

Biashara yenye ufanisi hutegemea uhakika wa huduma. Utendaji wetu wa kazi daima umelenga kutimiza matarajio ya wateja wetu. Hatuwezi kujifunga katika makataa yasiyoweza kutimizwa na wafasiri wetu.

Kotesheni

Tuma kazi yako kwa anwani yetu ya baruapepe huku ukibainisha makataa na lugha unazotaka zitafsiriwe. Hatuchukui zaidi ya dakika tano kujibu maombi yanayohusiana na kotesheni katika saa za kazi.

Languages spoken in South African provinces*

 Province (%) SA GP KZ WC EC MP LP FS NC NW
 IsiZulu 23 20 78   1 24 1 4 1 3
 IsiXhosa 16 7 3 25 79 1   8 5 6
 Afrikaans14 12 2 50 11 7 3 13 54 9
 English 10 13 13 20 6 3 2 3 3 4
 Sepedi 9 11       9 53     2
 Setswana 8 9 1     2 2 5 33 63
 Sesotho 8 12 1 1 3 4 2 64 1 6
 Xitsonga 5 7       10 17     4
 Siswati 3 1       28 1      
 Tshivenḓa 2 2         17     1
 IsiNdebele 2 3 1     10 2   1 1

*Data Statistics South Africa: Census in brief (2011) PDF

Wateja